Sunday 29 June 2014

Diamond Platnumz Baada Ya Kutofanikiwa Kupata Tuzo Ya BET Asema Haya

Imani yangu ni kwamba umekuwa mfuatiliaji mzuri wa habari tofauti kuhusu muziki wa Tanzania  na unafahamu kuhusu tuzo kubwa aliyokuwa akiwania msanii Diamond katika tuzo za Bet Nchini Marekani. Taarifa mpya ni kuwa Tuzo zimefanyika na Tuzo aliyowania Diamond ya Best Africa Act imekwenda kwa msanii mwenzake Davido kutoka Nigeria.
Kwenye instagram Ya Diamond Kuna Huu Ujumbe kuhusu Matokeo Hayo.
” Tusipopenda kukubali Matokeo na Ushindi wa Wenzetu basi Daima Hatutaweza kuwa Washindani….Muhimu ni kujua wapi tulipotoka na Wapi tulipo Leo… Katika Nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya Million 40, kuchaguliwa Tanzania ni fursa, Heshima na Hatua kubwa… Cha Muhimu ni kuitumia vyema Fursa Hii na Kuhakikisha Mwakani tunapiga Hatua Zaidi!…. Asante sana kwa wote wanaozidi kuni support kwa hali na Mali, Mapambano ndio kwaaaanza yanaanza sasa…..!!!!!! @wcb_wasafi For Life Baby
d

0 comments:

Post a Comment